Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Menina "Watu Wananiona Nina Roho Mbaya "Ila Nilipolia Hamkuwepo na Niliponyamaza pia Hamkuwepo.."

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


''Habari ndugu zangu Leo ningependa kuongea yale ya moyoni nafikiri kuna watu wananiona mimi kama mtu mwenye roho mbaya kwasababu nimerudi kufanya kazi lahasha napenda kuweka wazi kuwa nimepitia mambo mengi magumu sana, nilipolia hamkuwepo na niliponyamaza pia hamkuwepo.... Nilitukanwa saana nikayabeba au huenda kutokana na nature ya Kazi zangu naonekana kama na Party kumbe maskini ya Mungu ndio mfumo wa kazi yangu ili uingize pesa inabidi ucheke hata kama moyo unalia..... Nimejaribu kujiweka sawa Mungu amejua kuijenga Imani yangu na mwenye Imani hakufuru sitotetereshwa na kitu chochote abadani asilani..... Faraja Pekee niliokua nikiitegemea ni ya Mwenyezi Mungu na ndugu zangu wanaonipenda kwa haki, Ama kwa hakika Mungu hakupi mtihani akakunyima namna ya kuuvuka🙏🏻 Ni ngumu mimi kama binti teena ninae tegemewa kama muhimili wa familia nimekaa ndani miezi mitano na siku kadhaa bila kufanya kazi yoyote na kutumia akiba tuu, mimi nina mahitaji muhimu kama binaadamu kuna bills kuna ada za watoto na mengine mengi. Maisha sio marahisi kiasi cha kukaa ndani na maumivu kila siku, Jamani nilisha omboleza nilisha lia na Mungu wangu itoshe kusema Mungu ni mwema saana.... nimeona nitoke nijitafutie ni ngumu kukaa ndani muda woote huo. Hata mimi nina moyo na maumivu pia ila ili maisha yaende hatutakiwi kubaki na majeraha yenye kuzuia kusonga mbele... Hakuna mabadiliko ukiendekeza ASI bali kuna mabadiliko ukiizingatia CHANYA. Lawama fedhea, matusi, na mambo yoote ya maangamizi kila jambo baya ni langu mimi ndio fungu langu nalipokea lakini sitoacha kuwapenda woote mnaonipenda na mnaonichukia na kunitukana Mungu aliwaleta kwangu na mimi simpingi nawapokea woote kwa idadi Mungu anayo nikabidhi hata iwe kwa makundi... Nawapenda woote❤️hata wewe kama uliumbwa binaadamu la weza kukutokea lolote mitihani ni ya binaadam sio mawe wala vyuma kila mtu apokee lake analopewa na kushushiwa na mwenyezi MUNGU kwa maana hakuna limfikalo mja bila MUNGU kuliruhusu USIOMBE LIKUKUTE.. Sijawahi kuishi kwa kusikiliza maneno ya watu naishi kwa kusikiliza maneno ya Mungu..Sio kila mtu atanipenda hata Mungu yupo lakini kuna wasioamini kama yupo''

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments