Mex Cortez Afunguka "Ningechana Kingereza Motra Asinge Elewa Kitu"
Kitaa kinadai game ya Rap imechangamka na hii ikiwa blessed na wakongwe kama @mwanafa na @lordeyesmweusi baada ya Dis tracks kutoka kwa @motra_the_future na @mex.tz (Mex Cortez) kuachiwa, Motra akiwaita kikosi kazi WEUPE ikiwa ni kinyume cha WEUSI, kundi wanalobatle nalo kwenye game. Motra akiwakingia kifua Weusi na kuwadis Kikosi kazi.

Mex ni zao la Tamaduni music, kaingia studio na kumjibu Motra. akiwa kwenye Empire ya EFM, Mex amedai ameamua kumjibu Motra kwasababu hana hadhi ya kujibiwa na kikosi kazi,wale ni watu wazima hawawezi jibizana na mtoto kama Motra,hivyo akaona ngoja ajibu kwa niaba ya wakubwa.

Mex ni rapa anayeimba Bilingual yani kumix kiswahili na kiingereza, na mara nyingi amekuwa akiimba kiingereza lakini kaamua kutumia kiswahili kwenye Dis track sababu aliyotaja ni kuwa angetumia kiingereza Motra hasingeelewa.

Mex amedai ameona amkumbushe motra ni wapi katoka maana amejisahau kutukana watu waliomuinspire.

Hadi sasa kwenye Tab trending ya YouTube, Motra yupo namba 2 akiwa na siku nne huku Mex Cortez akikaa namba 5 akiwa na siku moja.

Kwenye Hizi Dis track mbili, ni yupi kamuua zaidi mwenzie.

By Sojamedia
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad