Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Miss Tanzania Kutoshiriki Miss World Kisa Hichi Hapa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Ikiwa zimesalia siku chache kufanyika kwa mashindano ya Miss World, mwakilishi wa Tanzania Juliana Rugamisa hatoweza kwenda sababu zikitajwa ni kukwama kwa viza.

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa leo Desemba 2, na uongozi wa kamati wa Miss Tanzania kwenye ukurasa wao wa Instagram, wameeleza hayo.

Mashindano ya Miss World ambayo mwaka huu yanatarajiwa kufanyika nchini Puerto Rico Desemba 12, mpaka sasa tayari wawakilishi kutoka nchi nyingine wameshawasili lakini mwakilishi wa Tanzania ameshindwa kufanya hivyo huku sababu ikitajwa kuwa ni kuchelewa kukosa viza.

“Hii ndio kusema kwa mwaka huu haitawezekana tena. Hata hivyo mwisho wa mashindano ndio mwanzo wa mashindano yajayo. Tunashukuru sana wadau wetu Miss World kwa jitihada kubwa na kuhakikisha hadi tunapata appointment mapema badala ya Januari, Serikali ya Puerto Rico ambao ndio wenyeji wa mashindano, umoja wetu wa 'country coordinators' dunia nzima imetufanya tumekua kitu kimoja badala ya kua washindani,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments