Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Mwili Waokotwa Shambani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ambaye amehitimu hivi karibuni aliyefahamika kwa jina la Magreth Mashue ameuawa na Watu wasiojulikana huku chanzo kikiwa bado hakifahamiki.

Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Mkoa wa Morogoro, Ralph Meela amesema Msichana huyo alikuwa anasoma Chuo Kikuu Cha SUA Kozi ya Sayansi ya Mazingira, alifanikiwa kufanya mahafali Novemba 26, 2021 na December 14 alipotea hadi December 18 mwili wake ulipopatikana katika mashamba ya Chuo hicho.

Meela anasema uchunguzi wa awali unaonesha shingo ya marehemu imelegea na kwamba huenda ikaww ndio chanzo cha kifo chake huku upelelezi ukiendelea kuwabaini waliohusika na kifo hicho ambapo hadi sasa wanamshikilia Mtu mmoja katika tukio hilo ambaye alikua rafiki yake wa kiume.

Kaimu Afisa Mawasiliano Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Scolastika Nduga amekiri kupokea mwili wa marehemu huku Kaka wa marehemu aitwaye Denis Mashue akiliomba Jeshi la Polisi kuwatafuta waliofanya tukio hilo ili wachukuliwe hatua za kisheria.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad