Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Mwanajeshi wa Kike Akamatwa Kwa Kukubali Kuvalishwa PETE ya Uchumba Akiwa na Nguo za Jeshi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Mwanajeshi wa kike amekamatwa nchini Nigeria kwa kukubali ombi la kuolewa akiwa amevalia magwanda rasmi ya kijeshi.

"Matendo yake yalikuwa yanazuia utaratibu mzuri na nidhamu ya kijeshi

"Kazi [ya wakufunzi] ilikuwa kuwafunza kikosi cha vijana na kutojiingiza katika uhusiano wa kimahaba na yeyote kati yao,"

Msemaji wa jeshi Jenerali Clement Nwachukwu aliiambia BBC kwamba mwanajeshi huyo alikiuka maadili ya jeshi, na pia sera yake ya mitandao ya kijamii.

Afisa huyu anatuhumiwa kukiuka kanuni za maadili za kijeshi kwa "kujiingiza katika mapenzi akiwa amevalia sare za jeshi la Nigeria",


Video ilisambaa mitandaoni wiki iliyopita ya askari huyo akipokea pete kutoka kwa mwanamume aliyepiga magoti mbele yake, huku watazamaji wakishiriki furaha ya wapenzi hao.


Kundi la kutetea haki za wanawake limeshutumu jeshi kwa kumbagua.

Wanadai Kuwa Hatua kama hiyo haikuwa imechukuliwa dhidi ya wanajeshi wa kiume waliohusika "katika maonyesho ya hadharani ya mahusiano ya kimahaba wakiwa wamevalia sare kamili za kijeshi", kikundi cha Women Empowerment and Legal Aid.


Mwanaharakati wa haki za binadamu na aliyekuwa mgombea urais wa Nigeria Omoyele Sowore alilaani uamuzi wa jeshi na kuuita "udhalilishaji".


Mwanajeshi huyo alikuwa amekubali pendekezo la ndoa kutoka kwa mwanafunzi katika mpango wa mafunzo kwa vijana wa serikali, anayejulikana kama Kikosi cha Huduma ya Vijana kwa Kitaifa (NYSC).


Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii waliwapongeza wanandoa hao, na kumsifu mwanamume huyo kwa kupendekeza. Wengine walimtania askari huyo.

NYSC bado haijatoa maoni.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments