Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Mwanamke aliyekunywa sumu baada ya kufumaniwa azikwa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURERombo. Mkazi wa kijiji cha Kibaoni, wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Shirima (26) aliyejiua kwa kunywa sumu ya kuulia magugu (Parasnow) baada ya kufumaniwa na mume wake aitwaye Riziki Shirima (22), amezikwa leo Desemba 15 nyumbani kwao baada ya mwili wake kukaa mochuari takribani siku 11.

Anna alifariki dunia Desemba 5 mwaka huu wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Huruma iliyopo wilayani humo baada ya kunywa sumu hiyo ya magugu iliyosababisha kifo chake.

Kattika tukio hilo, mumewe Anna (Riziki Shirima) anadaiwa kumuua mwanaume aliyemfumania na mkewe aliyejulikana kwa jina la Juvenal Claud kwa kumkata na mapanga baada ya kukutwa ndani nyumba yake na baada ya kumuua alijisalimisha mwenyewe polisi. 

Baada ya fumanizi hilo kutokea mwanamke huyo alikimbilia nyumbani kwa wazazi wake ambapo baadaye kutokana na fedheha aliyoipata alikunywa sumu ambayo ilipelekea kifo chake.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments