Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwanamke mwingine auawa ArushaKamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo
Arusha. Mwanamke mwingine mkazi wa Njiro jijini Arusha, Janerose Dewasi (66) ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali huku mfanyakazi wake wa ndani akituhumiwa kufanya mauaji hayo.

Tukio hilo ambalo limetokea siku chache baada ya mwanamke, Ruth Mmasi kubainika kuuawa eneo la Njiro mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea mauwaji hayo leo Jumatano Desemba 29, 2021 na kueleza kuwa linamsaka mfanyakazi wa ndani ambaye anatuhumiwa ambaye inadaiwa baada ya kufanya mauwaji hayo alitoweka.

Kamanda Masejo amesema mwili wa mwanamke huyo ambaye alikuwa anaishi na mfanyakazi huyo kwenye nyumba yake eneo la block D umekutwa amepigwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso.


 
"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa anaishi na mfanyakazi huyo wao pekee na alimuajiri wiki moja iliyopita" amesema

Amesema mara baada ya mauwaji hayo mfanyakazi huyo ametoweka na anaendelea kusakwa.

Kamanda amesema jeshi la polisi linatoa wito kwa wenye nyumba kuwa makini na wafanyakazi wa ndani wanaowapa kazi kwa kujua historia zao.


Mmoja wa majirani wa nyumba hiyo, Mary Muchi amesema mtuhumiwa huyo huyo alikuwa hajulikani sana mtaani kwani ameanza kazi muda si mrefu.

"Hatujui lolote huyo kijana anatajwa, alikuwa akiimsaidia huyu mama kazi zao na leo tumeshangaa kupata taarifa za kifo cha mama huyu"amesema.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments