Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Mwijaku Ampa Ushauri Zuchu "Yes mkamate kwa busara zitokazo kinywani mwako"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Moja kati ya headlines zinazo gonga vichwa vya habari mtandaoni ni issue inayomtaja mwanamuziki @diamondplatnumz kutaka kumuoa mwanamuziki mwenzake @officialzuchu , sakata ambalo kila mtu analizungumzia katika namna yake.

Sasa huenda sakata hili limemfikia mtangazaji kutoka clouds media, a.k.a. DC wa insta /maarufu kama msemaji wa maisha ya watu katika mitandao @mwijaku_01 baada ya kuandika ujumbe mrefu wenye mfano kutoka kwenye biblia ,ujumbe uliombatana na picha ya mwanamuziki Zuchu.

Katika post hiyo mwijaku alimaliza kwa kuandika maneno yanayo hisiwa kulenga sakata linalotajwa kuhusu #Diamondplatnumz kumuoa #Zuchu kwa kusema;

“Kuolewa na mtu sahihi sio kuomba tu, bali inaendana na uwezo wako wa kujitambua wewe binafsi, vipaumbele vyako visivyoathiri matakwa ya huyo mwanaume, kutambua mwanaume sahihi anapokuja kwako na kufahamu ni jinsi gani utamkamata kwa maneno matamu ya kinywa chako...Yes mkamate kwa busara zitokazo kinywani mwako!”✍@mwijaku_01

Je umeelewa alicho andika Mwijaku..!?


 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments