Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Nabii Shilla Awaponza Wasafi Wapigwa Faini Ya Mil 2 na TCRA

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
MAMLAKA  ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo Desemba 22, 2021 imetoa adhabu kwa Wasafi Media kutokana  na kurusha maudhui ya mahojiano kati ya Mwandishi wao Jordan Mwasha (Mchaga Og) na Daniel Shillah ambayo yalikuwa kinyume na sheria.

Maudhui ya mahojiano hayo yalipandishwa katika mtandao yao ya kijamii Novemba 1, 2021 yakiwa na kichwa cha HABARI; “HATA YESU ALIFATA WENYE PESA/MSITUITE MATAPELI”

Kufuatia kutenda kosa hilo, TCRA imetoa adhabu zifuatazo:

Kuwapa onyo kali, kuomba radhi watazamaji wake kupitia kituo chao cha Wasafi TV na Channel yao ya YouTube mara tatu kila siku kila baada ya saa nne kuanzia Desemba 23, 2021 mpaka Desemba 25, 2021 pamoja na kulipa faini ya shilingi milioni 2 ndani ya siku 21.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments