Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Polisi yamnasa mzee anayelewesha abiria

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREJESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael Abdul Said (68) mzaliwa wa Katoro mkoani Kagera kwa tuhuma za kuwalewesha abiria kwenye basi linalofanya safari kati ya Mwanza na Mara.

Matukio hayo yalishamiri mkoani humo tangu Oktoba mwaka huu ambapo watu tofauti waliripotiwa kuleweshwa na kuibiwa mali mbalimbali, huku ikihofiwa kuwa mihadarati iliyotumika ilitolewa kwa kiwango kikubwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, SP Longinus Tibishubwamu amesema mtuhumiwa huyo baada ya kukamatwa Disemba 02 mwaka huu, amebainisha kuwa wamekuwa wakitumia dawa ya kienyeji aina ya Kabharagata ambayo wamekuwa wakiiagiza kutoka nchini Kongo.

Amesema mtuhumiwa alikamatwa wilayani Bunda na kukiri kufanya matukio hayo katika mikoa tofauti ingawa alisema makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya. 

RPC Tibishubwamu amesema watamfikisa mahakamani wakati wowote, kwani mmoja wa abiria aliyewahi kuibiwa kwa mtindo huo katiba basi la Champion, amemtambua na mtuhumiwa amekiri kumfanyia uhalifu huo, mwezi uliopita

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments