Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Prince Dube, Tigere Waikosa Simba

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
NYOTA watatu wa Azam FC, Prince Dube, Never Tigere na Bruce Kangwa, huenda wakaukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba utakaochezwa wikiendi hii kutokana na kuwa na majukumu kwenye timu yao ya taifa ya Zimbabwe.


Wazimbabwe hao tayari wameungana na wenzao katika kambi ya kujiandaa na michuano ya AFCON
inayotarajiwa kuanza Januari 9 hadi Februari 6, mwakani nchini Cameroon.


Hivi karibuni, nyota hao ambao wanacheza kikosi cha kwanza cha Azam FC, wamejumuishwa kwenye kikosi cha awali cha Zimbabwe kabla ya kufanyika mchujo kesho Jumatano kupata kikosi ambacho kitashiriki AFCON.Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria, amesema: “Tigere, Kangwa na Dube
wameitwa katika timu ya taifa ya Zimbabwe kwa kambi ya muda kuchuja wachezaji watakaokwenda AFCON.


“Mchujo wao utafanyika Desemba 29, kama watafanikiwa kupenya, watasalia hukohuko, lakini wakishindwa, watarudi haraka kuuwahi mchezo dhidi ya Simba.”

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments