Rais Samia Suluhu "Pato la Mtanzania Lakifia Sh milioni 2.6 Kwa Mwaka, Jambo Hili Linaongeza Hadhi Yetu Machoni Mwa Mataifa"

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema wastani wa pato la mtanzania kwa mwaka 2020 ni Sh 2,653,790.

Akizungumza wakati wa kuhutubia Taifa, Rais Samia amesema takwimu hizo ni tofauti na mwaka 1961 ambapo wastani wa pato kwa mtanzania lilikuwa ni Sh 776.

“Jambo hili linaongeza hadhi yetu machoni pa jumuiya ya kimataifa na kutuondolea unyonge," amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, imechangia kuleta mafanikio makubwa, ikiwemo kuulinda uhuru wetu na mipaka yake, kujenga umoja wa kitaifa na mshikamano, kuimarisha uchumi wetu na kupunguza umaskini, na kuimarisha demokrasia.

"Katika eneo tunalopaswa kujivunia ni kuboresha maisha ya Watanzania na kuongeza upatikanaji wa huduma za jamii na ubora wake, kama sekta ya majisafi, elimu, afya na upatikanaji wa umeme,” ameongeza Rais Samia

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad