Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Simba Kuwakosa Wachezaji Saba Mchezo wa Kagera Sugar Yupo Morrison

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Simba ipo mjini Bukoba kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, huku ikiwakosa nyota wake tisa, wakiwamo Bernard Morrison na Rally Bwalya ambao kwa siku za karibuni wameonekana kuibeba timu hiyo katika mechi zao za kimashindano

Simba iliondoka jioni ya jana ikiwa na msafara wa watu 36 wakiwamo wachezaji 22, huku nahodha wake John Bocco akikosekana katika mchezo huo utakaopigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Kaitaba

Mbali na Morrison na Bwalya, wengine ni Chris Mugalu na Taddeo Lwanga ambao ni majeruhi wa muda mrefu , wengine walioachwa Dar ni; Erasto Nyoni, kipa, Jeremiah Kisubi, Israel Mwenda na Pascal Wawa

Meneja wa timu hiyo, Patrcik Rweyemamu amesema wachezaji hao tisa wameachwa kwa sababu mbalimbali ikiwamo kuwa majeruhi, kuugua na matatizo ya kifamilia, lakini jeshi lililopo Bukoba, lipo tayari kupeleka moto kwa Kagera ili kuendeleza wimbi lao la ushindi

Simba inashika nafasi ya pili katika msimamo na kama itashinda mechi ya kesho itaiengua Yanga kwa muda, kwani itafikisha pointi 21. Yanga inayoongoza msimamo imekusanya pointi 20 kupitia mechi nane kama ilizocheza Simba

Kukosekana kwa Bwalya na Morrison kutaipa ugumu Simba kwani nyota hao wawili kwa sasa ndio wanaoonekana kuipa uhai safu ya mbele ya timu hiyo kwa uwezo wao wa kumiliki mpira, kupiga pasi za mwisho na pia kuwavuruga wapinzani kwa vipaji walivyonavyo

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments