Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Simba SC kumuuza Ibrahim Ajibu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC huenda wakamtoa kwa mkopo Kiungo Ibrahim Ajib, katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili.

Ajibu anatajwa kuingia kwenye mpango huo, kufuatia kukosa nafasi ya kucheza chini ya Kocha Franco Pablo Martin ambaye amerithi mikoba ya Didier Gomes.

Hata hivyo bado haijafahamika ni wapi kiungo huyo atapelekwa kwa mkopo, lakini taarifa zinadai kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka Msimbazi.

Wachezaji wengine wanaotajwa huenda wakatolewa kwa mkopo ni Mlinda Lango Jeremiah Kisubi na Kiungo na Abdulsamad Kassim, ambao pia wamekosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.


 
Simba SC bado ipo kimya katika usajili wa wachezaji, huku ikielezwa kuwa huenda wakaweka wazi kila kitu baada ya kufanikisha mpango wa kuwatoa baadhi ya wachezaji wao kwa mkopo.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments