Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Skendo ya Walimu Kufanya Mapenzi na Wanafunzi Yatikisa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


MWAKA 2021 unapokaribia kutamatika, baadhi ya walimu wa shule mbalimbali wanauaga kwa skendo ya kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wao.

Kuna baadhi ya walimu walinaswa laivu wakiwafanyia uchafu na wanafunzi wao, baadhi waliwaoa kabisa na wengine kulalamikiwa kuwaharibu wanafunzi wa kike kimyakimya.

Ripoti ya Serikali ya mwaka 2021, imesema, walimu 285 kati 10,115 walifikishwa katika Tume ya Utumishi wa Ualimu (TSC) kwa tuhuma za kujihusisha na mapenzi na wanafunzi katika kipindi cha miaka minne.

Ripoti hiyo ilitolewa Septemba 7, 2021 na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu.

Skendo hii ya walimu kujihusisha kingono na wanafunzi wao ilithibitishwa pia na Mwenyekiti (TSC), Dk Willy Komba, jijini Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari.

Hali inavyoonekana tatizo la mapenzi kati ya walimu na wanafunzi linakua, wewe kama mwananchi unadhani nini kinasababisha na kipi kifanyike 2022, ili walimu viwembe washike adabu yao?

@manyota_rich

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments