Ticker

6/recent/ticker-posts

TOT Kusukwa Upya Kuendana na Ushindani wa MuzikiKatibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, Jumatatu 27 Disemba 2021 amefanya ziara fupi Kutembelea na kuzungumza na watumishi wa CCM wa kikundi cha Sanaaa Tanzania One Theater (TOT) Kinondoni Mwinjuma Dar Es Salaam


Katika ziara yake amesema Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan anatambua kuwa TOT ni moja kati ya Bendi kongwe nchini na yenye mchango mkubwa nchini, hivyo ameelekeza kufanya juhudi bendi hiyo iwe ya viwango vya juu


“Mwenyekiti anataka kuhakikisha utendaji kazi wenu uwe wa viwango vya juu kwa kuwa na vyombo bora na mazingira mazuri ya utendaji kazi ili muweze kuandaa tungo zinazoishi katika kujenga hamasa zenye kuakisi uhai, ukomavu na uimara wa CCM” alisema Shaka


Nae mkurugenzi mkuu wa bendi Ndugu Gasper Tumaini amesema Chama kupitia kwa Mwenyekiti Rais Samia kimezidi kuwajengea ari na ya kujituma zaidi


“Chama kinatupa matumaini makubwa juu ya kuimarishwa zaidi kwa bendi yetu na kuweza kutekeleza majukumu haya katika mazingira mazuri zaidi kama ilivyokua dhamira ya kuanzishwa kwake” alisema Tumaini


Bendi ya TOT ilianzishwa mwaka 1992 na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa lengo la kuleta hamasa ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi


Februari 5, mwaka 2022 CCM, itaadhimisha miaka 45 tangu kuanzishwa kwake Februari 5, mwaka 1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments