Ticker

6/recent/ticker-posts

Tutu Mwaka 1931 Hadi 2021, Dunia Inamlilia


Desmund Mpilo Tutu alizaliwa mnamo Oktoba 27, 1931, mauti yalimkuta Desemba 26, 2021, hadi anakata kauli alikuwa na umri wa miaka 90.

Tutu alizaliwa katika familia ya kimasikini ya Zachariahi huko Klerksdorp nchini Afrika Kusini.

Alisoma akawa mwalimu, baadaye alipata nafasi ya kwenda Uingereza kusoma zaidi katika nafasi ya uchungaji na akafanikiwa kuwa kiongozi wa Kanisa la Anglican.

Tutu amekuwa mtetezi wa haki za kupinga ubaguzi wa rangi huko Afrika Kusini, alifanikiwa kupata Tuzo ya Nobel.

Enzi za uhai wake, alikuwa ni rafiki mkubwa wa hayati Nelson Mandela, walishirikiana katika kuitetea Sauzi katika kuipatia uhuru wake.

Tutu alifanikiwa kufika hadi Tanzania na kukutana na hayati Benjamin Mkapa wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments