Ticker

6/recent/ticker-posts

Tuzo za Filamu Safi...Washindi Sio Majina Makubwa Tuliyoyazoea Bali ni Kazi Nzuri na Uwezo BinafsiUwenda majina yao si makubwa sana kwa wengi,na uwenda wengi tunawaona wakifanya kazi nzuri ila hatujui wanaitwa akina nani, Naweza sema tasnia ya Filamu nchini imepiga hatua,kuona ukubwa wa kazi ndio utafanya muigizaji kubeba tuzo na si nani ana jina kubwa apewe tuzo.

Isarito Mwakalindile, @isarito_tmt ambaye ni mshiriki katika tamthilia ya Jua Kali kabla ya Hapo akifanya poa kwenye tamthilia ya PANGUSO,ameibuka kuwa muigizaji bora wa kiume kwa mwaka 2021 huku tuzo ya Muigizaji Bora wa kike kwa mwaka huu, ikienda kwa mwanadada @godliver_gordian ambaye pia ni mahiri wa kuteka hisia za mtazamaji katika uhusika wowote ule, wengi wetu tukiwa tumemjua zaidi kupitia tamthilia ya Uhuru una gharama zake (2019) na kwasasa akiwa ni moja ya waigizaji katika Tamthilia ya Jua kali ambayo pia imechukua tuzo ya tamthilia bora ya mwaka 2021.

Hongereni Washindi, Endeleeni kupambania sanaa yetu.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments