Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Unaambiwa Sure Boy Amuondoa Mukoko Yanga

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


HUENDA kiungo mkabaji wa Yanga, Mkongomani, Mukoko Tonombe akatua kwa mkopo Azam FC katika usajili huu wa dirisha dogo

Usajili huo ulifunguliwa Desemba 16, mwaka huu na Yanga tayari imemtambulisha kiungo Salum Abubakari ‘Sure Boy’ aliyeomba kuondoka Azam FC.

Mukoko anatajwa huenda akatimka Yanga kwa kile kinachotajwa hana furaha ya kuendelea kukipiga hapo baada ya kukosa nafasi ya kucheza msimu huu.

Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, zinasema kwamba, Mukoko kwa kupitia menejimenti yake inayomsimamia, imeomba kiungo huyo aondoke kwa mkopo

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa Azam ndiyo timu ya kwanza kupeleka maombi ya kumtaka Mukoko kwa mkopo wa miezi sita aliyoibakisha katika mkataba wake ndani ya Yanga.

“Katika kuhakikisha analinda kipaji chake, uongozi wa Yanga huenda ukamtoa kwa mkopo Mukoko baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

“Hiyo ni baada ya menejimenti ya Mukoko kupendekeza mchezaji wao aondoke kwa mkopo na timu inayopewa nafasi kubwa ni Azam ambayo yenyewe imeonesha nia ya kumuhitaji.

“Kama mazungumzo yatakwenda vizuri, basi Mukoko atakwenda kwa mkopo Azam katika usajili huu wa dirisha dogo,” alisema mtoa taarifa huyo.

MUSA MATEJA NA WILBERT MOLANDI , DAR

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments