Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Usaliti wa Mwijaku somo kwa Harmonize

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
KITENDO cha mtangazaji na mwigizaji Mwijaku kuungana na msanii Diamond Platnumz na kuwa balozi wa kampuni yake ya michezo ya kubashiri, kinaelezwa kuwa ni usaliti kwa msanii Harmonize.
Mwijaku anafahamika kwamba ni sapota wa Harmonize hivyo baadhi ya watu wanasema kitendo alichokifanya ni usaliti mkubwa hivyo Harmonize anapaswa liwe ni somo kwa watu wengine wanaomzunguka.

Baadhi ya watu wanasema, kubwa la kujifunza ni kutoweka imani kwa binadamu mwenzako ukiamini atakuwa upande wake siku zote; tegemea tu siku moja binadamu mwenzako atakusaliti.

Jambo lingine linalotajwa kumfanya Mwijaku amsaliti Harmonize ni kutokana na jamaa huyo kuwa na mkono mfupi; yaani siyo mtoaji wa mkwanja wakati wahusika wanahitaji kuendesha maisha yao na familia zao.

Katika utetezi wake, Mwijaku anasema kuwa, yeye ni mweledi katika kazi yake ya ubalozi ukizingatia pesa nyingi alizowekewa mezani hivyo ilikuwa ngumu kuzikataa.


 
Hata hivyo, Mwijaku anaahidi kuendelea kumuunga mkono Harmonize na kumsoa Diamond pale atakapoona anastahili kukosolewa bila kujali kama ni balozi wa moja ya kampuni zake.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments