Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Uwoya: Nina Miaka 33 tu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREKAMA ilivyo kwa baadhi ya mastaa wengine wa kike Bongo kusababisha utata juu ya umri wao, mwigizaji Irene Uwoya naye amepita mulemule baada ya kutamka; “Nina umri wa miaka 33 tu…”

Uwoya ameyasema hayo wikiendi iliyopita alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ndani ya kiwanja cha bata ndefu cha Kidimbwi-Beach jijini Dar.

Kuhusu umri wake Uwoya anasema mwaka huu ametimiza umri wa miaka 33 kwani mwaka jana alitimiza umri wa miaka 32.

“Sijatimiza miaka 32, nimetimiza miaka 33 tu, mwaka jana ndiyo nilikuwa ninatimiza miaka 32…” anasema Uwoya; mama wa mtoto mmoja wa kiume, Krish aliyempata mwaka 2011 akimzalia aliyekuwa mumewe, marehemu Ndikumana.

Kuhusu ishu ya kula bata ndefu, Uwoya anasema wapo watu wanakula bata kuliko yeye, lakini yeye ndiye anaonekana zaidi.

“Mbona watu wanakula bat asana kuliko mimi? Labda kwa sababu mimi ndiye ninaonekana zaidi,” anasema Uwoya.

Kuhusu mwanaume anayempa jeuri ya kula bata, Uwoya anasema siyo mtu mkubwa kwa maana ya kiongozi mkubwa bali ni mtu wa kawaida sana na muda ukifika watafunga ndoa.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments