Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Wakati Makambo Akianza Kutupia Yanga..Mayele Apata Pancha, Aingia Uwanani Akichechemea

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Staa wa Yanga Fiston Mayele ni miongoni mwa watazamaji waliofika  jana Uwanja wa Benjamini Mkapa kushuhudia mchezo wa FA kati ya Yanga na Ihefu.

Mayele aliingia jukwaa kuu wakati mpira ni mapumziko na baada ya kuingia alisogea kusalimiana na baadhi ya viongozi wa Yanga.


Lakini wakati anatembea kuwasogelea viongozi hao alikuwa akichechemea kuashiria kwamba ana maumivu kwenye mguu wake.


Hali hiyo alionekana nayo pia wakati anaotembea kwenda kuketi kwenye kiti chake kwa ajili ya kutazama mechi.


Katika mchezo huo, Yanga waliweza kupata ushindi mnono wa magoli manne kwa bila, huku mshindani wa  Mayele kwenye kikosi cha Nabi, Herieth Makambo akifunga magoli matatu.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments