Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Walioshambulia gari la serikali ‘ kukiona’

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Walioshambulia gari la serikali ‘ kukiona’
MKUU wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo ameeleza kuwa wananchi waliohusika kushambulia gari la askari wa Wakala wa Hifadhi za Misitu (TFS) Mkoani Geita na kuwajeruhi baadhi yao watashughulikiwa.

Shimo amesema hayo katika mahojiano maalumu baada ya ufunguzi wa siku 16 za kupinga ukatili wilayani hapa. Novemba 27 mwaka huu, gari namba STL 3146 Toyota Land Cruiser mali ya TFS lilishambuliwa kwa mawe na wananchi wenye hasira kitongoji cha Lwamugasa, Kijiji cha Busolwa wilayani Geita.

Mkuu wa Wilaya alisema, kamati iliyoundwa kuchunguza undani wa tukio hilo tayari imeshakamilisha na kutoa taarifa kamili ambayo itaenda kufanyiwa kazi ikiwemo kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika.

Alisema vitendo vya aina hiyo havikubaliki kwani vinazuia askari kutekeleza majukumu yao hali inayorudisha nyuma juhudi za serikali kufikia lengo la kuhifadhi raslimali za misitu na wanyama.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments