Ticker

6/recent/ticker-posts

Wapiganaji wamchinja mchungaji Msumbiji
Wanamgambo wa Kiislamu wamemuua mchungaji mmoja wa kanisa katika wilaya ya Macomia, ilio na gesi nyingi katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgabo , kulingana na ripoti.

Jumatano iliopita, mkaazi wa kijiji cha Nova Zambezia alienda katika kituo kikuu cha polisi , akibeba mfuko uliokuwa na kichwa cha mchungaji huyo , chanzo kimoja cha kijeshi kimesema.

Wapiganaji hao wanaodaiwa kuhusika na Islamc state walimkamata mchungaji huyo katika uwanja mmoja, wakamkata kichwa na kumpatia mkewe kichwa hichona kumuagiza kuwaelezea polisi.

Hili ni shambulio la hivi karibuni kutekelezwa na Wanajihad ambao wamekuwa wakilenga wilaya kadhaa za mkoa wa Cabo Delgado tangu mwezi Oktoba 2017.


 
Wanamgambo hao hivi majuzi wamehamia mkoa wa Niassa , kufuatia wanajeshi waliopelekewa nchini humo na Rwanda, Msumbiji Pamoja na mataifa ya SADC.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments