Ticker

6/recent/ticker-posts

Watanzania Kweli Ngangari..Unaambiwa Asilimia 80 ya Waliougua Corona Hawakwenda Hospitali



Kwa mujibu wa Wizara ya Afya kupitia Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo ni kuwa tangu kuingia kwa janga la Corona mwishoni mwa 2019, asilimia 80 ya Watanzania waliopata Maambukizi hawakufika Hospitali huku asilimia tano walifikishwa ICU

Wizara imesema ukosefu wa Elimu ya kutosha kwa Wananchi umechangia Changamoto hilo, huku mpaka sasa mwamko wa chanjo ukisuasua katika maeneo mengi ikiwepo Mikoa ya Kanda ya Ziwa

Meneja wa Taifa wa Mpango wa Chanjo, Dkt Florian Tinuga ameyasema hayo wakati akitoa mafunzo maalumu kwa Waandishi wa Habari kuhusu kuripoti habari zinazohusu Corona. Serikali inatarajia kuzindua mpango wa pili wa Chanjo kitaifa kuanzia Desemba 22, 2021


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments