Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Watoto walionyweshwa sumu na Mama yao wafariki

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Watoto wawili kati ya watano walionyweshwa sumu na Mama yao Wilayani Chato Mkoani Geita wamefariki, imeelezwa walinyweshwa sumu ya kunyunyuzia nyanya na Mama yao Mzazi Veronica Gabriel (30) Mkazi wa Tarafa ya Buselesele .

RPC wa Geita Henry Mwaibambe amesema chanzo cha tukio hilo ni kutokana na ugumu wa Maisha ambapo Mama anadaiwa baada ya kuona maisha yao ni magumu aliona bora awaue Watoto wake na yeye mwenyewe kunywa sumu ambayo haikumuua.

“Watoto waliofariki ni Jane Mgema miaka 12 pamoja na Janeth Mkama miaka miwili, Watoto wengine watatu wamelazwa kituo cha afya Bwanga pamoja na mama yao (Mtuhumiwa) akiwa chini ya ulinzi wa Polisi, hali zao wote ni mbaya” ——— RPC.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments