Ticker

6/recent/ticker-posts

Watu wasiopungua 37 wamefariki Dunia baada ya moto kuzuka ndani ya kivuko


KIMATAIFA Watu wasiopungua 37 wamefariki Dunia baada ya moto kuzuka ndani ya kivuko kimoja kilichofurika abiria kusini mwa mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka.

Afisa wa polisi Moinul Islam amesema hadi sasa wamefanikiwa kupata miili ya watu 37 na wengi wao wamepoteza maisha kwa kuungua na moto huku wachache wamekufa maji baada ya kurukia mtoni.

Islam amesema inaaminika kuwa moto ulizuka kutoka kwenye chumba cha injini ya chombo hicho kilichobeba karibu abiria 500 badala ya uwezo wake rasmi wa kuchukua abiria 310.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments