Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Wolper "Hata Nikimfumania Baba Mtoto Wangu na Mwanamke Mwingine Simuachi"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
KUNA stori ambazo zimekuwa zikisambaa zikidai kwamba, baba mtoto wa mwigizaji wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper aitwaye Rich Mitindo eti alifumaniwa na mchepuko; mtoto mbichi pande za Kidimbwi kisha akatoka nduki na kuacha nguo ya ndani.

Sasa, stori hizo zimemkera mwanamama Wolper na kuamua kuwatolea uvivu wanaoeneza habari hizo akisema; “Hata kama akimfumania baba mtoto wake huyo, hawezi kumuacha kwa sababu hapo ndipo amefika…”

Wolper amelipuka; ““Nyie…(tusi) mnaotunga stori za uongo na kweli nataka niwaambie kitu kimoja, huyu niachieni kabisa ndiyo nimefika hapa, sina pa kwenda wala pa kugeuka na siku nikimkuta chumbani ndiyo nitampa adhabu tu kidogo, ila haachwi, sembuse kuniambia sijui Kidimbwi, sijui video, hamuoni kama mnapoteza muda wenu?


“Yaani mhusika nikimkuta chumbani, ninamshika mkono tunaenda nyumbani, tunapeana adhabu tunaendelea, je, nyie wa kuniletea maneno bila hata kanegative, nitawaelewa? Leteni video, leteni nguo yake ya ndani aliyoisahau kwa mchepuko, haachwi mtu hapa, nyie mnaosema muyasemayo, tatizo injini zenu mbovu, watoto wadogo mna…


(tusi) mumkome baba mtoto wangu…”Wolper na Rich Mitindo ni wachumba ambao miezi kadhaa iliyopita walijaaliwa mtoto wao wa kwanza wa kiume aitwaye Paskali, lakini kumekuwa na maneno mengi juu ya penzi lao huku baadhi ya wabaya wao wakisema; ‘wataachana tu…”

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments