Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Yaani Kumzuia tu Mke Wangu Kwenda Moshi X - Mass Hii Nimezua Ugomvi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


 

Jana ilitakiwa wife aende Moshi, ila nikaiminya hiyo ratiba. Nilimuambia aende Masasi ila hajaenda bado, analia mpaka muda huu anataka nimruhusu aende kwa wazee wake.

Na kwao yameibuka mapya, niliongea na shem wangu mmoja anasema agenda ni Mimi mwakani nikajenge Moshi, mimi si Mchagga na nimejenga kwetu Masasi, sasa naona hawa wakwe wanataka kunipanda kichwani.

Sioni ulazima wa kujenga Moshi, wazee wameibua mapya kabisa, na wife ananiambia kama safari hii simruhusu basi mwakani nikashushe mjengo Moshi, kwa hili nilimkatalia wazi wazi, na Moshi hatokwenda.

Hawa wazee nashindwa kuwaelewa, wanataka kunipelekesha nafikiri, kwa Mmakuwa mimi wamefeli sana!

Nai solve vipi hii ngoma watu wazima wenzangu?

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments