Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Zamaradi Amfungukia Irene Uwoya "Jini limezaliwa, halafu kadiri umri unavyoenda Jini linaongezeka makali"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Jini limezaliwa, halafu kadiri umri unavyoenda Jini linaongezeka makali!! nikukumbushe kidogo, siku ya kwanza nakuona ilikuwa Miss Mwanza 2007 nikiwa mshiriki, ulikuja kutembelea Kambini, sikumbuki kama kuna Shingo haikugeuka, Concentration ya mazoezi hata kwa Mamiss ikapungua, watu wote macho kwako, wanaume kwa wanawake, na hata baada ya kuondoka mjadala ukabaki, Watu wanajiuliza HUYU NANIIII!!! Mbona mzuri hivi!!! Na baadae tukakuona kwenye meza ya Majudge kama mmojawapo 😄

Ghafla kwenye sarakasi za maisha niko Clouds kipindi cha Filamu nikaona umeibukia kwenye OPRAH!!! Nyota Ikang’aa kwelikweli, kuna siku ulikuja kwenye Interview Take One watu wanatoka kuja kukuchungulia unafananaje!!! Nadhani sasahivi tumekuzoea tu ila kuna namna ulivyo especially kwa JICHO LA KWANZA LINALOKUONA!! 😄 hii ni story ndogo tu ya kukuonesha sio mimi tu ninaekuona, ila NDIVYO ULIVYO!!

Sasa Tokea Oprah mpaka leo Jini limeng’ang’ania namba, maana kuna namba fulani hivi kama TANO kwenye SHOWBIZ ya Industry ya filamu zina wenyewe (nitataja siku nyingine), miaka nenda rudi ziko palepale haziguswagi, mojawapo ni hii!!!

Happy Birthday My Darling!!! Nakupenda sana, na kwenye siku yako hii nataka tu ujue jambo moja..
WE MZURI!!!! Lakini pia Shukrani, nikushukuru kwa kuwepo kila nilipokuhitaji, we ni mwema kwangu na NINATHAMINI!! 🌹

Ikawe kheri, Baraka na mafanikio tele kwako na familia katika mwaka huu unaoanza

Happy Birthday to You Mama Krish @ireneuwoya8

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments