Ticker

6/recent/ticker-posts

Zuchu Naye Amtunishia Misuli Diamond Platnumz
JANUARI 30, mwaka huu msanii kutoka kiwanda cha Bongo Fleva, Zuchu aliachia wimbo wake wa SUKARI, ndani ya miezi 10 wimbo huo, umefanikiwa kugonga zaidi ya views milioni 60 na hii inamfanya kwa sasa kuwa msanii wa kwanza Tanzania mwenye wimbo wa peke yake (no collaboration) kufikisha idadi hiyo ya views.

Nyimbo zinazofwatia ni JEJE uliotoka mwaka 2020 wenye views milioni 59M na sikomi uliotoka miaka 3 nyuma wenye views milioni 53, zote za msanii Diamond Platnumz.

Hasa kupitia insta story yake, msanii Zuchu ameamua avimbe kidogo, “Ikumbukwe kuwa kwasasa yeye ndiye msanii wa kwanza tokea nchi ipate uhuru kuwa na wimbo (sio Kolabo) wenye views nyingi YouTube.”

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments