Ajifungua Mtoto Akiwa Na Umri Wa Miaka 11

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Pichani Victoria Ajey mwenye miaka 11 amejifungua mtoto wa kiume baada ya kubakwa na mume wa shangazi yake, mwanaume husika anaitwa Joseph Adoyi ambaye yupo kwenye miaka ya 50s na ni mlinzi wa chuo kikuu cha Benue.

Binti huyo alikuwa akiishi na shangazi yake tangu akiwa na miaka 3, alianza kubakwa na mume wa shangazi yake kisha mwanaume husika akawa anamtishia maisha mtoto huyo ikiwa angefungua mdomo kumueleza shangazi yake na ndipo mwishowe akapata mimba.

Shangazi yake alipogundua kuwa msala huo ni wa mume wake imeelezwa kwamba shangazi mtu akaamua kumrudisha kijijini mtoto huyo bila msaada wa kueleweka na yeye kuendelea na ndoa yake ambapo yeye na mume husika wamezaa watoto wakubwa ambao washamaliza vyuo.


Hata hivyo, Jamaa mmoja kwa jina la Andrew alipomuona mtoto huyo anateseka mitaani akiwa na ujauzito mkubwa bila uangalizi wa kueleweka ndio akaibukia Facebook kuelezea suala hilo ili wasamaria wema wamsaidie mtoto huyo ajifungue salama kisha kurudi shule kuendelea na masomo, pia kuvikumbusha vyombo vya sheria kumchukulia hatua mwanaume husika aliyempa ujauzito mtoto huyo.


 
Kwa mujibu wa media za Nigeria tayari mume wa shangazi yake ametiwa mbaroni na polisi baada ya sakata hilo kuwa hadharani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad