Barbara Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Sakata la Kuitwa Polisi "Amefungua Kesi ya Kijinai, Anadai Nimetumia Lugha Chafu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



“Siwezi sema niko vizuri lakini nipo okay, yule dada amefungua kesi, sijui nia yake ni nini, lakini nimesikitishwa sana kwa kweli, hii kitu haiko sawa.

“Amefungua kesi ya kijinai, anadai nimetumia lugha chafu, ukweli ni kuwa sijatumia lugha chafu, bahati mbaya Alhamisi nilishikiliwa siku nzima polisi kuhusu hilo suala.

“Sijaambiwa siku ya kurudi lakini polisi wanaendelea na uchunguzi, walikuwa wanatafuta ushahidi.

“Hata mimi mwenyewe nilishtuka nilipopigiwa simu mara ya kwanza na nilijua limeshaisha kwani nilipewa faini ya Sh laki tano na Bodi ya Ligi kwa tukio hilo la Desemba mwaka jana.

“Tupo kwenye ligi nilitakiwa kwenda Morogoro lakini hii kitu ilinichelewesha, kama ni lengo la kunichelewesha dada amefanikisha, lakini inaonekana hii vita ni kubwa.

"Tutaendelea kupambana, vita siyo uwanjani hata nje ya uwanja. Nitawapa ushirikiano polisi hadi litakapofika mwisho,” Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalenz akizungumza na Maulidi Kitenge, leo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad