Ticker

6/recent/ticker-posts


 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREBodi ya Wakurugenzi ya NBAA chini ya Mwenyekiti wake Profesa Sylvia S. Temu imeidhinisha matokeo ya watahiniwa 5,809  waliofanya mtihani mwezi Novemba 2021 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu  na Wakaguzi  wa Hesabu Tanzania (NBAA). Mitihani hiyo ilifanyika katika vituo 11 vya mitihani vilivyopo Tanzania Bara na Visiwani.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Pius  Maneno imebainisha kuwa matokeo hayo yanafuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 11 vya mitihani kutoka mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na Visiwani.

Alisema mitihani hiyo ilihusisha watahiniwa katika hatua ya kwanza na ya Pili katika ngazi ya cheti cha utunzaji wa  Hesabu (ATEC I , ATEC II) zenye masomo manne kila moja na ngazi ya taaluma, Hatua ya Awali/Msingi (Foundation Level) yenye masomo matano, Hatua ya Kati (intermiediate Level), yenye masomo sita na hatua ya mwisho yenye masomo manne(Final Level). Pia amesema Mitihani hii niya Kumi na tano Chini ya mfumo mpya wa elimu na Mafunzo unaozingatia weledi.

"Watahiniwa  waliosajiliwa  walikuwa  6,446  kati ya hao watahiniwa   637  sawa na asilimia  7.6  hawakuweza  kufanya  mitihani  hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo  watahiniwa   waliofanya   mitihani   walikuwa   5,809  sawa  na  asilimia 92.4. Kati ya watahiniwa hao 2,796 sawa na asilimia 48.1 ni wanawake na 3,013 sawa na asilimia 51.9 ni wanaume.

  Kati ya watahiniwa   waliofanya  mitihani  hiyo  watahiniwa   202 ambao ni asilimia 3.6  wamefaulu  mitihani  katika mkao mmoja, wengine  41 sawa na asilimia  0.7 wamefaulu  kwa  kufaulu  masomo  walioyokuwa   wameshindwa katika  mitihani  ya nyuma,  wengine  708  sawa  na  asilimia  12.2  wamefaulu mitihani  yao kwa  kufaulu  masomo  waliyokuwa   wamebakiza," alisema Maneno.   


 
Pia alisema  watahiniwa     961    sawa   na   asilimia    16.5   wamefaulu    mitihani    yao na kwamba watahiniwa   wengine   2,559  sawa  na  asilimia   44.1  wamefaulu   baadhi  ya masomo  katika  ngazi  mbalimbali  na watahiniwa  2,289  waliobakia   sawa na asilimia  39.4 hawakufaulu  mitibani  yao.

Amesema katika ngazi ya awali watahiniwa waliosajiliwa    walikuwa   742  kati  ya  hao watahiniwa   65  sawa na asilimia  8.8 hawakuweza   kufanya  mitihani hiyo kwa  sababu  mbalimbali na hivyo watahiniwa   waliofanya  mitihani kuwa  677   sawa  na  asilimia   91.2.     

Pia imeelezwa kuwa kati   ya  watahiniwa  677 waliofanya  mitihani katika ngazi hii watahiniwa  126  ambao ni asilimia 18.6 wamefaulu   mitihani  katika  mkao  mmoja huku mwingine  01  sawa  na asilimia   0.1  amefaulu   masomo   aliyokuwa ameshindwa katika mitihani ya nyuma na wengine 119 sawa na asilimia17.6 wamefaulu mitihani waliyokuwa wamebakiza.


Imeelezwa kwa ujumla watahiniwa  246  sawa na asilimia 36.3 wamefaulu mitihani yao ambapo watahiniwa 301 sawa na asilimia 44.5 wamefaulu baadhi ya masomo katika kazi hii na watahiniwa 130 waliobakia sawa na asilimia 19.2 hawakufaulu mitihani yao.

Aidha amesema katika hatua ya  Kati, waliojisaliwa walikuwa   3,379   kati  ya  hao watahiniwa  396 sawa na asilimia 11.7 hawakuweza   kufanya  mitihani kutokana na sababu  mbalimbali. Hivyo watahiniwa  waliofanya  mitihani walikuwa 2,983 sawa na asilimia 88.3.   Kati ya watahiniwa 2,983 waliofanya  mitihani  katika ngazi hii  watahiniwa   36 ambao ni asilimia 1.2  wamefaulu   mitihani   katika  mkao  mmoja,   wengine  35  sawa  na asilimia 1.2 wamefaulu  kwa  kufaulu  masomo waliyokuwa wameshindwa  katika  mitihani  ya  nyuma.

Alisisitiza kuwa wengine 313 sawa na asilimia 10.5  wamefaulu  mitihani yao kwa kufaulu  masomo waliyokuwa  wamebakiza, hivyo  kwa   ujumla   watahiniwa    384  sawa   na asilimia 12.9 wamefaulu  mitihani yao. Watahiniwa 1,446  sawa  na asilimia    48.5   wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi  hii. Watahiniwa    1,153  waliobakia   sawa  na  asilimia   38.5  hawakufaulu mitihani  yao.

Katika hatua ya mwisho, waliosajiliwa walikuwa 2,076 kati ya hao watahiniwa 163 sawa na asilimia 7.9 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanua mitihani walikuwa 1,913 sawa na asilimia 92.1. Kati ya watahiniwa 1,913 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 29 sawa na asilimia 1.5 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 04 sawa na asilimia 0.2 amefaulu kwa kufaulu masomo aliyokuwa ameshindwa katika mitihani ya nyuma.


 
Amesema watahiniwa    236  sawa   na asilimia   12.3  wamefaulu   mitihani   yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza ambapo Watahiniwa    269  sawa  na asilimia    14.0 wamefaulu mitihani yao huku watahiniwa 713 sawa na asilimia 37.3 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi  hii. Watahiniwa    913   waliobakia    sawa   na   asilimia   48.7   hawakufaulu mitihani  yao.

 Maneno amesema kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA imetoa pongezi kwa wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka wale ambao hawajafuzu kutokata taama badala yake waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili wawezo kufuzu mitihani ijayo.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments