Ticker

6/recent/ticker-posts


 

BREAKING NEWS: Moto unaunguza Bunge la Afrika Kusini

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURECape Town. Moto mkubwa unaunguza jengo la Bunge la Afrika Kusini lililopo jijini Cape Town.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, moto huo umeanza leo Jumapili Januari 2, 2022 alfajiri.

Kikosi cha zimamoto nchini homo kipo kwenye eneo hilo kikipambana kuuzima moto huo ambao bado chanzo chake hakijafahamika.

Moto huo umetokea saa chache baada ya mazishi ya Askofu wa kwanza mweusi Muanglikana aliyesaidia kukomesha ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, Desmond Tutu yaliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu George ambalo lipo karibu na jengo hilo la bunge.

Bado moto huo haujadhibitiwa ingawa zimamoto wanaendelea kupambana kuuzima.

Hakuna taarifa za vifo wala majeruhi zilizoripotiwa

Taarifa zaidi kukujia……

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments