Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Godbless Lema "Kumekuwepo na Matukio Mengi ya Hatari Nchini"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREAliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema kuwa inabidi ufanyike utafiti wa haraka wa afya ya akili za watu, kufuatia uwepo wa matukio mengi nchini ya watu kujiua, watoto kuua wazazi wao ama wazazi kuua watoto wao.

Rai hiyo ameitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, hii leo Januari 14, 2022.


“Kumekuwepo na matukio mengi ya hatari nchini, watu kujinyonga, watoto kuua wazazi, wazazi kuua watoto pia na ulevi wa kupindukia, kuna hitajika utafiti wa haraka wa afya ya akili za watu, ugumu wa maisha na kupoteza matumaini kumeongeza msongo wa mawazo na uchungu, ni hatari sana, “– ameandika Lema

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments