Hizi ndo Akili za Baadhi ya Wanawake....Huyu Anaomba Ushauri Baada ya Kuingia Chaka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





HUYU DADA ANAOMBA USHAURI

Jamani naombeni ushauri wenu, sijui nifanye nini. Mimi ni binti wa miaka 23, nipo chuo mwaka wa tatu. Naomba ushauri wako, mwaka jana nilikua na mpenzi wangu, ni mwanafunzi mwenzangu, lakini tukagombana tukaachana na yeye akamchukua rafiki yangu. Nikiwa katika maumivu nilikutana na mwanaume mwingine ambaye naye pia ni mwanafunzi mwenzangu.

Alinisaidia sana kupona kwenye maumivu yangu, alikua ananijali, ananisikiliza na kila kitu ananifanyia. Kaka nilikua vizuri sana, tukajikuta tumeingia kwenye mahusiano naye na mpaka sasa tuna miezi sita. Kaka sababu ya kuja kwako ni hivi, baada ya kuona kuwa X wangu hanijali, amemchukua rafiki yangu niliamua kumkomoa, nikabeba mimba ya huyu Kaka ambaye niko naye.

Kweli nilimuambia na alikubali akanipeleka mpaka kwao, shida kaka inakuja sasa hivi nina ujauzito wa miezi minne. Nyumbani hawajui kama nina mimba, X wangu amesikia kuwa nina mimba na kunitafuta ili tuongee. Kusema kweli kaka nilikua na hasira naye ila aliponitafuuta nilihisi kuchanganyikiwa, kwanza nililoana kabisa, yaani niliona kama dunia imefunguka.


 
Nilikubali kuonanana naye, ingawa nilijaribu kuficha lakini alitaka tufanye mapenzi akaona tumboa langu nikawa sina namna zaidi ya kumuambia kuwa nina mimba ya mwanaume mwingine. Huwezi amini kaka X wangua liumia sana na kuniambia kuwa ananipenda na sikutakiwa kuzaa kwasasa, kusema kweli nimekaa na kufikiria sitaki kuzaa hasa na huyu mwanaume niliyenaye kwani nahisi simpendi.

Sababu ya kuja kwako ni hivi, X wangu anataka kunirudia na anataka kunioa, ameshanivalisha pete ingawa si sherehe ila kanivalisha na akaniambia nitoe hii mimba ya huyu mwanaume kisha nibebe mimba yake kwani ananipenda na hataki nirudiane na huyu mwanaume. Kaka naomba ushauri, namuachaje huyu kaka kwani kanisaidia sana.

Kumpenda simpendi ni ile tu wakati ule nilikua nashida, sitaki kumuumiza nawaza nimuacheje ili asiumie. mimba yake nimeshaitoa na imeenda vizuri ingawa ilikua ni kubwa, lakini ninachotaka kujua sasa namuachaje, yeye sasa hivi yuko kwao na kila siku ananipa naongea na wazazi wake kuhusu mtoto yaani nashindwa nini chakufanya, sitaki kumuumiza kama nilivyoumia mimi hata sijui nifanyaje jamani nipo njia panda.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad