Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Huenda Kanye West Akaenda JELA Kwa Kosa la Kumpiga Shabiki yake Magumi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREVyombo mbali mbali ulimwenguni,ukiwemo mtandao mkubwa wa habari wa @tmz_tv ambao umeripoti kuwa, Idara ya Polisi jijini Los Angel wanafanya uchunguzi kuhusiana na shtuma zinazo mkabili rapa @kanyewest baada ya kumpiga Shabiki aliyekuwa akiomba saini (autograph) ya Rapa huyo. Mashtaka hayo yamefikishwa asubuhi ya Leo Alhamis kwa saa za Marekani katika idara ya polisi jijini Los Angel.

Hii inakuwa si mara ya kwanza Kanye West kukutana na zahama hii, ambapo mwaka 2014 alishtakiwa kuhudhuria session 24 za Anger Management (menejimenti ya saikoloji kuhusiana na mambo ya hasira) na kufanya kazi za kijamii kwa masaa 250 baada ya mwaka 2013 kuvunja Camera ya Paparazi aliyejulikana kwa jina la Daniel Ramos.

Kanye West bado hajakamatwa kuhusiana na ishu hii, na endapo atakutwa na hatia, basi anaweza kwenda jela kwa miezi 6.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments