Huku Simba Ikiwa Bado na Machungu...Mo Dewji Tajiri wa 15 Afrika Takwimu za Forbes kwa mwaka huu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



WAKATI mashabiki wa Simba wakisumbuliwa na msongo wa mawazo kutokana na matokeo mabaya waliyopata hivi karibuni Rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ametajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 18 wa Afrika kwa ripoti ya mwaka 2022.

Simba kwenye mechi mbili za mwisho kabla ya mchezo wa leo na Kagera Sugar wameambulia pointi moja baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City na kuambulia suluhu na Mtibwa Sugar.

Katika orodha hiyo ya jarida la Forbes kwa mwaka huu limemtaja MO kuwa bilionea namba 15 akifungana na matajiri wengine wawili Othman Benjelloun na Youssef Mansour wote wakiwa na utajili sawa.

Utajiri wa Mo umetajwa kufikia Dola bilioni 1.5 (Sh3.4 trilioni) utajili ambao ni sawa na mwaka jana hivyo hajaongeza wala kupunguza.


Katika orodha ya jarida hilo mwaka jana Mo ambaye ni raia wa Tanzania anayefanya biashara mchanganyiko alikuwa nafasi ya 15 akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.5 (3.4 trilioni).

Uwekezaji katika viwanda vya nguo, unga wa ngano na sembe, mafuta ya kupikia, sabuni, sukari na vinywaji unatajwa kama chanzo cha utajiri huo wa Dewji ambaye kwa hapa Tanzania yeye pekee ndiye ameingia katika orodha hiyo ya mataikuni 18 barani Afrika.

Kwa kuingia katika orodha hiyo, Dewji anafuata nyayo za Mmiliki wa Mamelodi Sundowns, Patrice Motsepe amabye yeye ana utajiri unakadiriwa kufikia Dola 3 bilioni (zaidi ya Sh 9 trilioni)


Pia Dewji ndiye mtu pekee kutoka Afrika Mashariki aliyeweza kuingia katika orodha hiyo kwa mujibu wa Forbes huku nchi za Afrika Kusini, Nigeria na Misri zikitawala.

Aliko Dangote aliyewekeza katika biashara za sukari na simenti anashika nafasi ya kwanza akiwa na utajiri wa Dola 13.9 bilioni na anafuatiwa na Johann Rupert & family mwenye utajiri wa Dola 11 bilioni huku nafasi ya tatu ikishikilia na Nicky Oppenheimer wa Afrika Kusini mwenye utajiri wa Dola 8.7 bilioni.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad