Ipo Wapi Zamani...? Mpo Wapi Watu wa Zamani Mje Muone Mioyo ya Watu ilivyobadilika!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


*IPO WAPI ZAMANI?*

Zamani Nyumba Zetu Zilikua Vyumba Kidogo na Sehemu ya Kukaa tu, Tunakutana Ndugu, Jamaa na Majirani.
Lakini Leo Nyumba Zetu Kubwa na Zina Vyumba vingi, isipokuwa Hazina Watu ila Ardhi na Kuta tu.

Zamani Chakula Chetu ni Wali, Mihogo, Ndizi, Magimbi, Dagaa la Kitonge, au Ugali kwa Chukuchuku.
Tunatandika Mkeka au Jamvi Chini na Tunakula Sahani Moja Sote, Tunacheka kwa Furaha Mpaka Jirani Wanatusikia.

Lakini Leo hii Sufuria au Hotpot Imejaa Nyama, Kuku na Minofu ya Samaki na Kila Mmoja na Sahani Yake ya Aina Tofauti .

Zamani Tulikuwa Tunakwenda Shule kwa Kupitiana Nyumba Hadi Nyumba, Mnafika Shule Mnahesabu Namba na Kukimbia Mchaka Mchaka
Lakini Leo hii Watoto wanapitiwa na school Bus Wakifika Shule Hakuna Mchaka Mchaka, Hakuna Kuhesabu Namba..

Zamani Tunakaa Uwani na Babu, Anatuhadithia Hadithi, Tunakunywa chai kwa upendo na Kucheka kwa Pamoja kwa Tabasamu Mpaka Meno Yetu Yanaonekana.

Lakini Leo hii Kukaa Kwetu ni Kwenye Simu za Mkononi, Internet na Kuchat tu Kwenye Whatsapp, Wechat, Instagram, Facebook na Mitandao Mengine ya Kijamii, Tumekua Tupo Kwingine Kabisaa.

Zamani Tunauliziana, Kujuliana Hali, kutembeleana, na Tunakutana kwa Furaha na Kukumbatiana.

LAKINI Leo Hii ni Sikukuu Mpaka Sikukuu au Harusi had harus au Mpaka Kuwe na Maziko Ndio Tunatembeleana au Kuonana Tena Kwa Kujilazimisha

Zamani Mtu Akiumwa Kati Yetu, Tunakusanyika Ndugu na Majirani.

Lakini Leo hii Ndugu Hakujali, hana Muda na Wewe.

Zamani ilikua Ndugu Anamuenzi Ndugu Yake na Dada Yake, Kwa Kila Alichonacho Hata Kama Kachoka au ana Msongo wa Mawazo.

Lakini Leo hii Unamkuta Mtu Hapati Kula na Ndugu Yake Yupo Kazama katika Neema, Anajifanya Kakasirika kwa Sababu Zisizoeleweka, na Kukata Mawasiliano kwa Miaka. Hajali Ndugu Wala Jirani, UTU Unapotea Anasahau kama Kuna Kufa au Dunia ina Mwisho .

Zaman mtu akimaliza shule anapata ajira. Lakini leo hii mtu akimaliza chuo hapati ajira, anasota mitaan kuzunguka na vyeti na cv na barua ili apate kazi but kazi hazionekani. . Ajira ni za kujuana tu. Wanaajir kindugu na wakati mwingine ANAKUAMBIA utoe rushwa kidogo upate kazi au mukutane kimwili ili upate kazi. Inasikitisha sana.

Mpo Wapi Watu wa Zamani Mje Muone Mioyo ya Watu ilivyobadilika!!

Miaka na siku Hazirudi NYUMA , TENDA Wema Uende Zako Usingoje Shukrani.

Hamna tena undugu wa kuwakusanya pamoja kama zamani, hamna mapenzi na upendo ndani ya mioyo, (Hata heshima kwa mkubwa kama zamani hamna).

Iko wapi zamani? Mola awarehemu wa zamani waliotangulia. Waliojenga upendo undugu ktk jamii, waliondoa udini, tuliishi kwa furahaa na Amani, sikukuu zote tulikuwa tunashirikishana Pamoja

*Mwenyezi MUNGU Atujaliye Tuwe Wenye Kupendana na kushikamana kwa Kila Hali kama ilivyokuwa ZAMANI.*

*UMOJA WETU NDIO UNDUGU WETU....!*
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad