Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Kesi ya Sabaya na Wenzake Mahakama Imeamua Hivi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewakuta na kesi ya kujibu watuhumiwa saba wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi akiwamo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Leo Ijumaa Januari 14, 2022 Hakimu Mkazi anayesikiliza kesi hiyo namba 27 ya mwaka 2021, Patricia Kisinda amesema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 13 wa Jamhuri na vielelezo 12 mahakama imeona washitakiwa wote saba wana kesi ya kujibu.

Akitoa uamuzi huo mdogo, Hakimu Kisinda amesema baada ya mahakama kupitia vielelezo hivyo na mashahidi vilivyotolewa kuthibitisha makosa yanayowakabili na baada ya kujiridhisha imeona washitakiwa wote wana kesi ya kujibu

Akiongea kwa niaba ya Washtakiwa wote, Wakili wa upande wa utetezi wakili Moses Mahuna amesema watakuwa na Mashahidi wasiopungua kumi na watajitetea chini ya kiapo.

Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wanatuhumiwa kuchukua fedha shilingi milioni 90 kutoka kwa Mfanyabiashara Francis Mroso kwa madai kwamba amekwepa kodi.

Watuhumiwa katika kesi hiyo ni lengai ole sabaya,Silvesta Nyegu,Enock Togolane Mkeni,Watson Mahomange,John Odemba,Nathan Msuya na Jackson Macha

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments