Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Lukuvi Kushirikiana na Waziri Mkuu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURESiku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kusema kuwa atamvuta Ikulu aliyekuwa Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, leo Januari 13, 2022 Rais Samia amesema kiongozi huyo atakuwa akisaidiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kusimamia sekta zenye migogoro baina ya viongozi.

Akizungumza na mawaziri na manaibu katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Rais amesema hatua hiyo ni baada ya kugundua baadhi ya viongozi hawana maelewamo katika utendaji, hali inayopelekea kufanya kazi bila ushirikiano.

“Waziri na naibu wake migongano, mnagombaniana safari, ooh safari ilikuwa yangu anakwenda yeye mimi hanipi, wakati sekta ni kubwa, kila mtu akashika eneo lake mkafanya kazi, migongano yenu siielewi, wakati mwingine mnagombana kwa maslahi,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa weledi na kuepuka malumbano na kufanya kazi pamoja na kuongeza kuwa viongozi hao wanapaswa kuheshimiana hata moja wao anapokosea.


“Kama mwenzako ana tatizo, mwite kistaarabu, mweleze siyo kutukanana. Siyo njoo hapa wewe una…nitakwenda kumwambia mama, hapana rekebishaneni kwanza huko. Mkianza kutunishiana misuri na kutishana, hatuwezi kufika,” amesema Rais Samia Suluhu Hassan.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments