Ticker

6/recent/ticker-posts

Madai Mazito Yaibuka Country Boy Kusepa Konde Gang
SIYO stori tena kwamba, msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mandingo almaarufu Country Boy ameachana na Lebo ya Konde Music Worldwide; lebo inayomilikiwa na msanii Harmonize, lakini stori mpya kuna madai mazito nyuma ya pazia.

Licha ya Harmonize kuiweka taarifa hiyo hadharani kwa kumuaga rasmi Country Boy siku ile ya Januari januari 9, 2022, zipo tetesi za msanii huyo kusepa Konde Music ambazo zilianza kuenea kwa kasi kote mitandao mapema jioni ya Januari 7, 2022.

Kuna madai mazito kwamba, kabla ya Country Boy kusainiwa Konde Gang alishafanya kolabo na msanii wa lebo moja hasimu na lebo hiyo.

Inasemekana kwamba, Country Boy alipoingia Konde Gang aliambiwa aweke mezani ngoma alizonazo na mojawapo ni hiyo.


Inadaiwa kwamba, menejimenti waliigomea ngoma hiyo kwenda hewani hivyo mwamba akawa anaisikiliza mwenyewe tu kwenye ndinga na magetoni.

Za ndani kabisa zinadai kwamba, stori hizo zilifika kwa mejimenti kuwa Country Boy anavujisha ngoma kwa watu kinyume na makubaliano na akaonywa.

Tetesi zinasema kuwa, ishu hiyo ilimfanya Country Boy kupata moto kwa kuwa anaamini ngoma hiyo ndiyo itampeleka zaidi mjini na kumfanya awe kwenye kilele cha mafanikio.


Ilidaiwa kwamba, ishu nyingine ni kwamba mwamba alitaka awe anapiga shoo kila kukicha, lakini kila mapromota walipoleta dili la shoo hata kama ni za ndondo za mikoani, menejimenti ilizipiga chini kwa madai kwamba dau ni dogo.

Za ndani kabisa zinadai kwamba, hapo ndipo jamaa alipoona isiwe kesi, akamvaa Konde Boy akaomba kusepa kwa makubaliano ya pande zote.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments