Mgeja: Soko kuu la Dodoma libadilishwe jina lisiitwe Job Ndugai

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MWENYEKITI wa Taasisi ya Mtanzania Mzalendo Foundation Hamisi Mgeja, ameiomba Serikali kubadilisha jina la Soko kuu la Dodoma kutoitwa tena jina la Job Ndugai.

Amebainisha hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, muda mchache mara baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, kuandika barua ya kujiuzulu nafasi yake.

Mgeja ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga ,amesema jina hilo linatia kichefuchefu kuendelea kuonekana kwenye Soko kuu la Dodoma, kwa madai ameinajisi nchi na kulidharirisha Taifa, kwa kumpinga Rais Samia Suluhu Hassani, juu ya mikopo ambayo inachochea maendeleo ya nchi, kutokana na ulafi wake wa madaraka.

"Kitendo alichokifanya Ndugai hata kumbukumbu zake kwenye lile Soko kuu la Dodoma Jina lake halifai kuwepo pale liondolewe kabisa, na kuweka jina jingine, sababu linatie kichefuchefu," alisema Mgeja.

Katika hatua nyingine, aliwataka pia watu ambao alidai kuwa ni wafuasi wa Ndugai kujithamini katika nafasi zao.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad