Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Mimi Mars na Marioo Kama Nandy na Billnass

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


ZIPO kapo mbili za mastaa wa Kibongo ambazo zinatajwa zitakuwa ni pambe mno kwa mwaka 2022. Kapo hizo zinahusisha ile iliyonoga zaidi mwishoni mwa mwaka 2021 ya mrembo Nandy au The African Princess na jamaa yake, Billnass au Nenga.

Unaweza kusema ni kama mahaba yao yalizaliwa upya baada ya kufunga safari mpaka huko Dubai ambako walikwenda mapumzikoni na kufurahia penzi lao.

Wapenzi hao wa muda mrefu waliamua kwenda Dubai; moja ya miji ya starehe duniani na kutembelea maeneo mbalimbali kama jangwani na kula bata.

Kapo nyingine ni ile ambayo imekuwa ikisemwasemwa zaidi, lakini sasa inaelekea pazuri kama Nandy na Nenga inayowahusisha mrembo Mimi Mars na Marioo au Toto Badi.

Ukiiacha na Nandy na Nenga ambayo huwenda ikazaa matunda mwaka huu; kwa maana ya ndoa na mtoto, kumekuwa na tetesi nyingi na za muda mrefu kwamba Mimi Mars na Marioo ni kitu na boksi; yaani wanatoka kisela kama ule wimbo wa dada wa Mimi Mars, Vanessa Mdee wa Kisela.


Katikati ya tetesi hizo, hatimaye Marioo ameanza kukoleza wino mwekundu katika tetesi hizo kuonesha ishara kuna mambo mekundu yanaendelea kati yao.Marioo amejibu ujumbe wa Mimi Mars wa kumtaki heri ya kuzaliwa kwa kuweka emoji ya kopa (love) na kusababisha emoji za watu waliotokwa na macho na zile za moto kuwa kama zote huku wakisifiwa kuwa kapo yao ni pambe mno.

Hata hivyo, mara kadhaa wawili hao wamekuwa wakitupilia mbali tetesi hizo pindi waulizwapo katika mahojiano mbalimbali.

“Happy birthday Chiee (jina ambalo Mimi Mars anamuita Marioo), Mwenyezi Mungu akujaalie miaka mingi zaidi uendelee kutoa hits na kuniandikia hits, Enjoooooy your day Marioo…” aliandika Mimi Mars Ijumaa iliyopita akimtakia Marioo heri ya kumbukumbu ya kuzaliwa.Kama utakumbuka, Mimi Mars ambaye ni Mpare amewahi kumshirikisha Marioo ambaye ni Mndengereko katika wimbo wake wa Una ambao alikuwepo pia Young Lunya.

Kama ambavyo Nandy ambaye ni Mpare naye amewahi kumshirikisha Nenga ambaye ni Mchaga kwenye nyimbo zake kadhaa kama Do Me na Party hivyo kuwepo kwa mfanano kwa asilimia nyingi.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments