Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Mukoko: Napitia Magumu Yanga

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
KIUNGO nyota wa Yanga kwa msimu uliopita, Mukoko Tonombe ameweka wazi kuwa anapitia magumu ndani ya
timu hiyo kwa sasa baada ya kutokuwa na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza.

Tonombe aliweka wazi hilo baada ya kuandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao ulionyesha kutokuwa na hali nzuri baada ya nafasi yake ya kucheza kuwa finyu.


Ujumbe wa Mukoko ulikuwa wa pande tatu, moja kuwashukuru Watanzania na Wanayanga kwa kumsapoti toka amefika nchini, ujumbe mwingine ulihusu nia yake ya kutaka kufanikiwa akiwa Yanga na mwingine ukionyesha matumaini ya kuyashinda majaribu.

Tonombe aliandika: “Asante sana Mungu wangu kwani umefanikisha ndoto yangu hapa Tanzania kuja kunipa vikombe vyote.

“Asante sana shabiki wangu wa Yanga natumai bado hata maisha yamekuwa magumu ila nitafanikiwa. Naamini na namshukuru Mungu sana.”


Mukoko kwa sasa anakabiliwa na ushindani wa namba baada ya timu hiyo kuwasajili viungo Khalid Aucho na Yannick Bangala.

Stori: Issa Liponda, Dar es Salaam

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments