Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Mwanamuziki Bien wa Sauti Sol Afunguka Kuporwa Vitu Vyake

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Mwanamuziki nyota wa kundi la Sauti Sol la nchini Kenya, Bien Aime, anadai ameiibiwa kwenye tamasha la ‘NRG Wave’ lililofanyika usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya katika viwanja vya Carnivore.

Mapema Jumamosi ya Januari mosi 2022, Bien ameutumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuweka bayana namna tukio hilo la kuibiwa lilivyotokea.

Amesema kwamba alinyakuliwa na kupoteza simu pamoja na funguo za gari yake ikiwa ni miongoni mwa vitu vingine vya thamani alivyopteza.

“Simu hiyo ilikuwa na sauti zangu zote za hivi majuzi za albamu inayofuata ya Sauti Sol,” alisema.

Na kupitia ujumbe wake aliouweka kwenye mtandao wa Twitter, Bien ametoa zawadi ya Ksh.50,000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 1 za Kitazania, kwa yeyote atakayefanikiwa kurejesha vitu vyote alivyopoteza.

“Nimeshangaa sana kwani huenda nisiwe mtandaoni mwezi mzima. Yaani jana ningekaa vibaya mgeniibia hadi bibi!. Nitatoa zawadi ya pesa taslimu 50K kwa ukizirudisha,” aliongeza Bien.

Katika hafla hiyo ambapo Bien anadai aliibiwa, alikuwa miongoni mwa wasanii wa Kenya waliokuwa wakitumbuiza pamoja na mkali wa dancehall wa Jamaica Konshens aliyetua na kupokelewa kwa shangwe nchini Kenya siku chache kabla ya Tamasha hilo.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments