Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Navy Kenzo Wamepotea Kwenye Ramani ya Muziki Bongo

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Hawa watu wamepotea wapi? mbona walikuwa na Uwezo mkubwa sana, Walikuwa wanaiwakilisha vizuri Tanzania pia walichangamsha sana game. Kwasasa Game limepoa sana, Imagine Harmonize, Mond na Kiba wanatikisa nchi kizembezembe tu bila ushindani wowote kutoka kwa wasanii wengine.

Popote walipo wasikie kilio hiki, warudi haraka sana kwenye game na wawe serious pia, game bado linawahitaji, game limetawaliwa na watu wachache tu hasa WCB, naamini wakirudi hawa Competition itarudi.

Vanessa kaacha muziki, hawa pia hawaeleweki, Alikiba anaelekea ukingoni, duuh! BongoFleva inaelekea wapi?

Halafu, kwanini NavyKenzo wamepotea baada tu ya kufanya Collabo na Mond "Katika" maana baada ya hapo wanatoa ngoma lakini kama haziendi hivi! Au wamefanyiwa Figusu, maana muziki ni vita Muraaa!

By @Hopetygatz

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments