Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Nyumba 21 zaezuliwa Kilombero, wananchi wakosa makazi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREKilombero. Baadhi ya wananchi katika katika kata ya Kalengakelu Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro hawana sehemu ya kuishi baada ya nyumba 21 na madarasa matatu ya shule ya msingi Kalengakule kuezuliwa na upepo.


Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Jumapili Januari 2, 2022 Mkuu wa Wilaya ya Kilombero (DC), Hanji Godigodi amethibitisha kutokea tukio hilo.

Amesema kuwa mpaka sasa hakuna taarifa za watu kupoteza maisha

“Ni kweli nyumba 21 zimeezuka lakini hakuna mtu aliyepoteza maisha” amesema DC Hanji

Amesema kuwa upepo huo umeezua madarasa matatu na ofisi moja ya walimu.

“Kwa upande wa shule kuna madarasa matatu na ofisi, vitabu vilivyokuwemo mule hakuna kilichoharibika” amesema

Mkuu wa Wilaya ameagiza wataalamu kufanya tathimini ya haraka kwa kushirikiana na kamati za maafa za kata na vijiji ili wananchi wapate msaada.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments