Ticker

6/recent/ticker-posts

Rais Samia "Kuna Wanaochoma Makusudi Sababu Wana Bima Watalipwa"


"Mioto hii ina sababu kadhaa, Kariakoo tuliambiwa hitilafu ya umeme, Karume ripoti ya awali tunaambiwa mishumaa lakini hata moto unapoendelea magari yakiwa yanakuja hayana maeneo ya kupita na kwenda kuzima moto, tujipange ili magari yaweze kupita kwa urahisi, wale wanaopika kuna ile 'nabandika maharage kesho nikija nitakuta yameiva' inawezekana kabisa moto ukashika kitu moto ukaendelea "

"Lingine ni suala la Bima kuna wale ambao labda amekata Bima ya biashara yake lakini kwa miaka kadhaa hajafaidi matunda ya Bima yake kwahiyo anaamua tu 'ngoja niweke kicheche cha moto hapa kukiungua Mimi kwasabau nina Bima nitalipwa na Bima' hilo nalo lipo"

"Jingine ni hawa wanaochukua mizigo madukani inawezekana Mtu kachukua mzigo mkubwa kauza, moyo wa ushetani unamtuma asiende kurudisha, weka moto mwenye duka atajua soko limeungua au karume imeungua kwahiyo sina cha kulipa na huenda mwenye duka ana bima atalipwa huko, ndio maana nimesema tumekua sasa tujisimamie" " ——— Rais Samia akizungumza na Viongozi wa Wamachinga Dar es salaam leo

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments